ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 2, 2024

CDF MKUNDA AELEZA UMUHIMU WA JKT KATIKA ULINZI WA TAIFA




MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akikagua gwaride kabla ya kufunga mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba



MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akikagua gwaride kabla ya kufunga mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba

MRADI WA RUWASA KUZINUFAISHA KAYA 164 ZA RUVU STESHENI KUPATA HUDUMA YA MAJI

 


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 

Kaya zipatazo 164 zilizopo katika  eneo la  Ruvu station lililopo  Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani wameondokana na changamoto ya maji baada ya kukamilika kwa mradi wa kisima cha maji chenye uwezo wa kutoa lita 11,820.

Akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Meneja wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) Debora Kanyika alisema kwamba kisima hicho kitakuwa na urefu wa mita 43.

Meneja Kanyika alibainisha kwamba mradi huo ambao utekelezaji wake ulianza tangu mwaka 2023 una uwezo wa kuhifadhi maji lita zipatazo elfu 50,000 juu ya mnara wa mita 12.

Kadhalika Meneja huyo alibainisha kuwa mradi huo wa kisima utakuwa na na vituo vipatavyo saba ambavyo ni kwa ajili ya kuweza kuchotea maji.

"Mradi huu una urefu wa mita zipatazo mita 43 na kwamba mnara wa mita 12 pamoja na vituo vipatavyo saba vya kuchotea maji kwa wananchi sambamba na mitambo ikiwa na mitambo ya kutandaza mabomba yenye kipenyo cha kuanzia inchi tatu hadi robo tatu,"alisema Meneja huyo.

Kadhalika alisema kwamba mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi milion 328 kupitia mfuko wa Taifa wa maji wa (NWF).

Aidha Meneja huyo aliongeza kuwa utekelezaji wa mradi  umeongeza hali ya upatikanaji wa maji kwa asilimia moja kwa Wilaya ya Kibaha na sasa huduma hiyo imefikia asilimia 78.

Pia alifafanua kwamba mradi huo ni moja ya utekelezaji wa kampeni ya Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kumtua ndoo mama kichwani.

Katika hatua nyingine Meneja alibainisha kwamba mradi huo umeweza kutoa fursa ya ajira kwa wananchi wapatao 63 ambao wanatoka katika maeneo mbali mbali ya Wilaya Kibaha.

Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Godfrey Mzava ameridhishwa na meadi huo wa maji na kuwapongeza kwa dhati uongozi wa Ruwasa kwa kazi ambayo wanaifanya katika kuwahudumia wananchi.

Kadhalika aliwahimiiza viongozi wa Ruwasa kuhakikisha kwamba wanayafanyia marekebisho baadhi ya mambo katika mradi huo ikiwemo upatikanaji wa Jenereta.

CCM IRINGA WAWAPONGEZA WALIMU WAZALENDO

 

Katibu Siasa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM mkoa wa Iringa, Joseph Ryata akiongea na walimu wazalendo wilaya ya Kilolo mkoani Iringa

Na Fredy Mgunda, Iringa 

CHAMA cha Mapinduzi CCM mkoa wa Iringa kimewpongeza walimu wazalendo kufundisha kwa juhudi na kumuunga mkono Rais Dr Samia suluhu Hassan katika kutekeleza ila ya CCM ya 2020/2025 kwa vitendo.


Akizungumza na walimu wazalendo Katibu Siasa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM mkoa wa Iringa, Joseph Ryata alisema kuwa walimu wamekuwa na mchango mkubwa wa kimaendeleo kutokana na kutoa elimu kwa wote na mara nyingine kuwaelimisha wazazi umuhimu wa elimu.


Ryata alisema kuwa walimu wanaaminiwa na jamii kutokana na elimu,burasa na maarifa wanayotumia kwa jamii wanayoishi nayo kwa kuwaelimisha mambo mbalimbali ya kimaisha na kimaendeleo.


Alitumia wasaa huo kuwataka walimu kusaidia serikali kuyaelezea mambo makubwa yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kutoka ushauri wenye hoja za kujenga kwa viongozi wa Chama na Serikali katika maeneo wanayoishi ili kuhakikisha ilani ya CCM inatekelezwa ipasavyo kwa maslahi ya wananchi.


Ryata amewapongeza walimu hao kwa umoja na uamuzi wao mzuri wa kuunda na kujiunga katika jukwaa la Walimu Wazalendo huku akisema Mwanachama au Kada wa CCM asipokuwa Mzalendo hawezi kuwa na tija ndani ya CCM na hawezi kufaidika vyema na fursa mbalimbali ndani ya Chama hicho na nchi kiujumla. 


Sambamba na hilo, Ryata amewataka walimu hao kuendelea kuielimisha jamii na kusimamia maadili, misingi ya utoaji Elimu Bora na Malezi kwa watoto ambao ndio wanafunzi wao wanapokuwa shuleni.

 

Kwa upande wao walimu wazalendo wamekipongeza chama cha Mapinduzi (CCM)mkoa wa Iringa kuendelea kuwapa ushirikiano na kutambua mchango wao katika jamii huku wakiomba Uongozi  uzidi kuwapambania na kuzisema kero na changamoto zinazowakabili walimu katika utumishi.

WATUMISHI WA TAWIRI WAUNGANA NA WAFANYAKAZI DUNIANI KUADHIMISHA SIKU YAO ADHIMU

 

WATUMISHI wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI)  Mei Mosi 2024 wameungana na Wafanyakazi Duniani kote kuadhimisha Siku yao adhimu ambapo kitaifa maadhimisho yanaendelea katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijinu Arusha na Mgeni Rasmi wa Sherehe hizo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango

TAWIRI tunajivuni mchango mkubwa wa watumishi katika kusimamia, kuratibu na kufanya tafiti za wanyamapori nchini kwa ustawi wa uhifadhi na kukuza utalii nchini. 

Aidha, Kauli mbiu ya siku hii ya Wafanyakazi Duniani kwa mwaka huu ni *"Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha"*




 Kauli mbiu ya siku hii ya Wafanyakazi Duniani kwa mwaka huu ni *"Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha"*

KIBAHA DC WAPITISHIWA MIRADI YAO YOTE 13 NA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA


 NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 


Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani imeweza kupata baraka baada ya kiongozi wa  mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka 2024 Godfrey Msava kuridhishwa na kupitisha miradi yote 13 ya mandeleo.

Kiongozi huyo wa mbio za mwenge kitaifa amepitisha miradi yote  hiyo 13 ambayo  imepitiwa na mwenge wa uhuru na kuwapongeza viongozi mbali mbali ambao wameweza kuhakikisha wanaisimamia vema na kutumia fedha vizuri ambazo zimetolewa  na serikali kwa kuzingatia mfumo wa kidigitali.










Alisema kwamba licha ya kuridhishwa na miradi hiyo mbali mbali ya maendeleo lakini ameagiza baadhi ya miradi ambayo imeonekana kuna na dosari  kadhaa wahakikishe wanazifanyia kazi na kuzirekebisha.

"Nawapongeza viongozi wote wa halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kwa kuweza kutekeleza miradi yenu kwa vitendo na kitu kikubwa fedha ambazo zinatolewa na serikali zitumike vizuri katika kutekeleza miradi ya maendeleo "alisema Mzava

Kadhalika aliongeza kuwa Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan anatenga fedha kwa ajili ya miradi mbali mbali ili kuwasogezea huduma wananchi hivyo viongozi na watendaji wanapaswa kusimamia miradi hiyo kwa maslahi ya wananchi.

Mwenge wa uhuru umepita katika miradi mbali mbali ya maendeleo ambapo umekagua mradi mkubwa wa kongani ya viwanda 
ya  SINOTAN, uliopo Kata ya Kwala ambao  utagharimu kiasi cha shilingi  trilioni 8.4. mpaka kukamilika kwake.

Pia Mwenge huo wa uhuru umeweka jiwe la msingi katika  mradi wa ujenzi wa barabara kutoka barabara ya Morogoro kwenda ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha yenye urefu wa mita  zipatazo 300  ikiwa katika kiwango cha lami.

Aidha mwenge wa uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha pia umepitia miradi mingine ya maendeleo ikiwemo uzinduzi wa  zahanati ya Vikuruti ambayo itakuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo.

Kadhali iliweza kuzindua mradi mkubwa wa maji ambao unatekelezwa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira(RUWASA) ambao umegharimu kiasi cha shilingi 328.

Sambamba na hilo mbio za Mwenge wa uhuru umeweza kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika sekta mbali mbali ikiwemo,afya,elimu,maji miundombinu ya barabara mapambano ya rushwa ukimwi,lishe pamoja na miradi mingine ya maendeleo.

Awali akiupokea Mwenge wa uhuru Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon alibainisha kwamba Mwenge huo katika Halmashauri mbili za Kibaha mji na Wilaya ya Kibaha utazindua jumla ya miradi 28 yenye thamani ya shilingi trilioni 8.5.

Nao baadhi ya wananchi ambao waliweza kupata fursa ya kushiriki katika mbio hizo wameshukuru Mwenge wa uhuru kwa kuweza kuzindua baadhi ya miradi na mingine kuweka mawe ya msingi ambayo kwa upande wao ni mkombozi mkubwa katika kuwasaidia huduma muhimu za kijamii.

Tuesday, April 30, 2024

'HAYA NDIYO NILIYOYAKUTA NDANI YA HIFADHI YA MAKUMBUSHO YA AZIMIO YA ARUSHA'

 NA ALBERT G. SENGO/ ARUSHA

Napata fursa ya kutembelea Makumbusho ya Azimio la Arusha yaliyoko eneo la Kaloleni, karibu na Mnara wa Uhuru (Mnara wa Mwenge). Hadi mwaka 1967, jengo hili lilitumika kama ukumbi wa ustawi wa jamii kwa jamii ya Kaloleni jijini Arusha. Mnamo Januari 1967, jengo hilo lilikuwa na mkutano wa kihistoria ambao Sera ya Kisiasa na Kiuchumi ya Tanzania ya Ujamaa na Kujitegemea ilitolewa. Mnamo Februari 1977 jengo hilo lilibadilishwa kuwa jumba la kumbukumbu ndogo la kisiasa na uchumi. Jeh ni yapi yaliyomo ndani ya Makumbusho haya? Ungana nami msimulizi wako Albert G. Sengo nikupitishe hatua kwa hatua katika eneo hili ambalo ni nyenzo muhimu ya kufundishia kwa historia, kiraia, masomo ya jumla na masomo ya sayansi ya siasa.

ZEE LA NYETI AJILAUMU KIFO CHA GADNA - "UKISIKIA MTU ANAUMWA USIAHIRISHE NENDA KAMSABAHI"

 NA ALBERT G. SENGO/ ROMBO, KILIMANJARO

Mwandishi wa Habari za Burudani na Michezo wa Gazeti la Mwananchi ambaye pia ni Mtangazaji na Mjasiliamali, Henry Mdimu 'Zee la Nyeti' amezungumza na Jembe Fm wakati wa mazishi ya mwanahabari nguli wa Clouds Fm, Gadna G. Habash, jinsi alivyoguswa na msiba wa marehemu huyo aliyefariki asubuhi ya Jumamosi ya tarehe 20 April 2024 baada ya kuugua na kulazwa katika Hospitali ya Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam. Mdimu ameiasa jamii kutopuuzia suala la kwenda kwa wakati kuwajulia hali wapendwa wao wanapougua kwani yeye aliahirisha mara kadhaa kwenda kumtembelea hospitalini marehemu Gadna wakati alipopata taarifa za kulazwa kwake. "Nimejuta Gadna wiki moja kabla ya kifo chake nilikuwa nafanya show Morogoro kwahiyo tuklikuwa tumeshaelewana, tumeshalipana hela ya tangazo lakini kesho yake nikasikia jamaa amelazwa, nikawaambia stuff wangu msimsumbue huyu jamaa kwasababu nimetoka naye mbali, tutakuja kufanya naye tangazo siku nyingine na nikirudi Dae es salaam nitakuja kumwona" "Nimeenda Dar es salaam nimekaa siku tatu, sikupata nafasi ya kwenda hospitali lakini nilikuwa napiga simu kwa marafiki, jamani kuna mtu amekwenda kumwona Gadna?'" Jibu - "Yes" Swali - "Anaendeleaje?" Jibu - "Yuko Powa" "Basi nikasema niende tena Morogoro nikirudi nitamkuta, nafika tu Morogoro nasikia Gadna amefariki"............ #samiasuluhuhassan #mwanza #rombo #gadna

MKE WA MBUNGE JIMBO LA KIBAHA MJI ATIMIZA AHADI YAKE KWA VITENDO VIJANA WA HAMASA

 


NA VICTOR MASANGU KIBAHA 


Jumuiya ya Umoja wa vijana ya Chama cha mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Kibaha mji umempongeza kwa dhati mke wa Mbunge wa  Jimbo la Kibaha mji Selina Koka kwa kuona umuhimu wa kuwasapoti vijana kwa kutoa  msaada wa  mahitaji na vitu  mbali mbali ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake alizozitoa  kwa vijana.


Pongezi hizo zimetolewa na Katibu wa UVCCM Wilaya ya Kibaha mjini Gamalu Makona wakati wa halfa fupi ya kukabidhiwa baadhi ya mahitaji na vitu mbali mbali kwa ajili ya kuwasaidia vijana wa hamasa ambao wapo katika mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na  kuupokea Mwenge wa uhuru.
Aidha Katibu huyo alisema kwamba Mama Koka amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia mambo mbali mbali katika jumuiya ya vijana katika Jimbo la Kibaha mji.

Aliongeza kwamba Mama Koka amewashika mkono na kuwapatia msaada wa vyakula mbali mbali,sambamba na mabati viti meza kwa ajili ya ujenzi wa banda ambalo litakuwa linatumika kukutana vijana wa uvccm pamoja na kupumzikia ili kujadili mambo ya jumuiya na maendeleo.

"Kwa kweli tunamshukuru na kumpongeza Mama Koka kwa kuwa na upendo wa kipekee maana hivi karibuni alikuja kututembelea umoja wetu na kile ambacho alituahidi kiukweli amekitekeleza na Mungu aweze kumbariki yeye pamoja na Mbunge kwa kuwa na moyo wa kujitolea,"alisema Katibu.

Akikabidhi msaada huo wa vitu mbali mbali kwa niaba ya Mama Koka Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Method Mselewa alisema kwamba msaada huo ni moja ya utekelezaji wa ahadi ya mke wa Mbunge kwa vijana hao ambayo aliitoa alipokwenda kuwatembelea hivi karibu.

Katibu Method alisema Mama Koka anatambua mchango mkubwa ambao unafanywa na jumuiya ya vijana hivyo akaamua kutoa mahitaji mbali mbali ambayo yatawasaidia vijana pindi wanapokuwa wakiendelea na mazoezi yao ya kujiandaa na Mwenge wa uhuru.

Mselewa alibainisha kwamba vijana hao ni Taifa la kesho hivyo wanapaswa kupendana na kuwa na maadili mazuri pamoja na  uzalendo kwani ndio viongozi watarajiwa katika siku za usoni.

"Hapa nimekuja kwa niaba na mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mama Koka na nimekuja na vitu mbambali kwa ajili ya chakula pamoja na redio ambayo mtakuwa mkiitumia katika burudani na mambo mengine,"alifafanua Katibu huyo.

Aliwahimiza vijana kuendelea kufanya mazoezi pamoja na kushiriki kikamilifu katika kuupokea Mwenge wa uhuru ambao utatembelea miradi mbali mbali ya maendeleo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nikson Saimon ambaye naye alifika kuwajulia hali vijana hao wa hamasa amewahimza kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika ujio wa mapokezi ya mbio za Mwenge wa uhuru na kwamba serikali ipo pamoja nao.

Katika hatua nyingine aliwaahidi katika mkesha wa mwenge kutakuwa na burudani mbali mbali za wasanii wakubwa pamoja na wasani wa kibaha na kwamba siku hiyo wategemee kuona burudani ya aina yake hivyo wajitokeze kwa wingi.

MWENGE WA UHURU WATOA BARAKA KWA RUWASA MRADI WA MAJI FUKAYOSI UENDELEE

 


NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO


Wananchi wapatao elfu 3666 katika kijiji cha Kidomole  pamoja na vitongoji vyake mbali mbali vilivyopo katika  kata ya Fukayosi  Wilayani Bgamoyo Mkoa wa Pwani wanatarajia kuondokana na changamoto ya usumbufu wa majii fikapo mwezi Mei mwaka huu baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji ambao utakuwa ni mkomboz mkubwa kwa wananchi hao.

Hayo yamebainishwa na  Meneja wa wakala wa Usambazaji wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) Wilaya ya Bagamoyo  James kionaumela wakati akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge  wa Uhuru  kitaifa ndugu  Godfrey Mnzava kuhusiana na utekelezaji wa mradi huo ambapo alisema kwa sasa upo katika hatua za mwisho kwa ajili ya upanuzi.


Meneja huyo alibainisha kwamba unatekelzwa chini ya mkandarasi mzawa AM&Partiner Limeted na Building Contractors kutoka jijini Dar es Salaam na kwamba kwa mujibu wa mkataba huo mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo Mei 11 mwaka huu.

Alifafanua kwamba katika upanuzi wa mradi huo pia unakwenda sambamba na ujenzi wa  tibio la maji katika eneo la Saadan na kwamba mradi huo umegharimu kiasi cha   zaidi ya  shilingi milioni 603 ambazo ni fedha kutoka katika mfuko wa maji( NWF)





Meneja huyo alibainiha kwamba utekelezaji wa mradi huo ulianza rasmi mnamo tangu Mei 11 mwaka 2023 na pia utaweza kuzinufaisha kaya zipatazo 796 kutoka kata ya Fykayosi pamoja na vitongoji vyake wananchi wataweza kuondokana na changamoto ya maji na hatimaye kupata huduma ya maji safi na salama.

Pia alisema kuwa katika kutekeleza mradi huo umeweza kutoa fursa mbali mbali za ajira kwa vijana wa lika mbali mbali  wapatao 50 ambao kwa sasa wameweza kujipatia kipato halali na kujikwamua kiuchumi.

Meneja huyo alibainisha kwamba katika eneo la kijiji cha Kidomole utekelezaji wa mradi huo umefikia kwa kiwango cha asilimia 90% ikiwa ni pamoja na ujenzi wa tanki kubwa lenye ujazo wa lita elfu 50,000 kwenye mnara wa mita 12.

Katika hatua nyingine Meneja huyo alitoa shukrani za dhati kwa Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha anatenga fedha katika kuboresha sekta ya maji kwa vitendo lengo ikiwa ni kuwapatia huduma wananchi ya maji safi na salama.

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Mnzava pamoja na wakimbiza mwenge wenzake wameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo na kukubaliana kwa pamoja kuupitisha pamoja na kuwapongeza Ruwasa kwa kazi nzuri ambazo wanazifanya katika kuwapelekea huduma ya maji wananchi.

Alisema kwamba huduma ya maji ni muhimu sana kwa wananchi hivyo Ruwasa waendelee kuchapa kazi kwa bidii na kuhakikisha wanatekeleza miradi ya maji kwa kiwango ambacho kinastahili kulingana na fedha ambazo zinatolewa na Rais.

Monday, April 29, 2024

MIRADI YA TRILIONI 8.5 KUTEMBELEWA NA MWENGE WA UHURU MKOA WA PWANI.

 

VICTOR MASANGU,CHALINZE


Mbio za Mwenge wa Uhuru umewasili leo rasmi mkoani Pwani ukitokea Mkoani Morogoro ambapo umekabidhiwa kwa Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambapo utembelea na kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo.

Akipokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge alisema kwamba katika mbio hizo mwenge huo utatembelea jumla ya miradi ipatayo 126.


Kunenge alibainisha kwamba mbio za Mwenge huo wa uhuru kwa mwaka huu  utakimbizwa katika Halmashauri tisa zilizopo katika Wilaya saba  ambapo jumla ya kilometa 1,225.3 zitakimbizwa katika maeneo mbali mbali.

Kunenge alifafanua kwamba kati ya miradi hiyo miradi 18 itawekewa mawe ya msingi,miradi 22 itazinduliwa na miradi ipatayo 86 itakaguliwa.

Aidha Kunenge alisema kuwa miradi hiyo itagharimu  kiasi cha shilingi Trilioni 8.536  ambapo serikali kuu imechangia bilioni 13.6,Halmashauri za wilaya shilingi bilioni 2.3 nguvu za wananchi na wawekezaji trilioni 8.5 na wadau wa maendeleo bilioni 14.6.

Pia alimshukuru Rais wa awamu ya sita kwa kuweka mazingira bora kwa ustawi na ufanisi zaidi katika sekta binafsi nchini.


Pia Kunenge katika hatua nyingine alisema kwamba katika kupambana na janga la ukimwi wameendelea kupambana kwa kutoa elimu ya upimaji wa wenza.

Kadhalika aliongeza katika kupambana na dawa za kulevya wameendelea kuimarisha mapambano kwa kubadilisha fikra,hisia na tabia.

Awali kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Godfrey Mnzava alizitaka halmashauri zote za Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanaandaa nyaraka zote za miradi ya maendeleo.8

Saturday, April 27, 2024

DOZI MOJA INATOSHA KUFANIKISHA KUZUIA SARATANI SHINGO YA KIZAZI.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

NI maadhimisho ya ‘dozi ya chanjo ya HPV’, inayomkinga mtoto wa kike asipate ugonjwa wa saratani ya mlango wa shingo ya uzazi.

Chanjo hiyo ya HPV inawalenga watoto wenye umri kati ya miaka tisa na 14, ambayo Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, anasema kuwa dozi moja inatosha kumkinga msichana kupata ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi. 

Waziri Ummy anayaongea hayo kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya Dozi moja ya chanjo ya HPV kwa wasichana, akinena ni jukumu la wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka watoto kupata chanjo hiyo. 

Ni hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Furahisha Wilayani Ilemela, Mwanza akiwa na ufafanuzi: “Wataalamu wetu ambao wanatoka kwenye Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). 

“Wametuhakikishia kuwa dozi moja ya chanjo ya HPV inatosha kumkinga msichana kupata saratani ya mlango wa kizazi.” 

Anasema awali dozi zilitolewa mbili, ya pili ikiwa ni miezi sita akipelekewa binti, hata hivyo wengi hawakurudi kumalizia. 

Lakini anaeleza mbadala uliopo ni kwamba, hivi sasa anasema wanatoa dozi moja, inayotosha kuwakinga wasichana dhidi ya maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi.  

Waziri anaeleza saratani inayoongoza kuwatesa Watanzania ni ‘Mlango wa Kizazi’ anayosema katika kila wagonjwa100, wako 23 wagonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi.  

Anaorodhesha saratani zinazofuatia kwa ukubwa ni inayohusu: Mfumo wa Chakula, asilimia 11; matiti asilimia 10.4; tezi dume asilimia 8.9. 

Pia, Waziri anatoa wito kwa wazazi na walezi nchini, kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo zote wanazopaswa, ili wanufaike na kinga dhidi ya maradhi yaliyotajwa, ikiwamo lengo kubwa la kuwakinga na magonjwa, yakiwamo haya ya saratani pamoja na kuwakinga na vifo vinavyoweza kuzuilika na chanjo.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi.

  

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Saidi Mtanda atahakikisha watoto wote wenye umri wa kuanzia miaka tisa hadi 14, wanapata chanjo hiyo ili kufikia malengo.  

“Kwa mwaka 2022/23 Mkoa wa Mwanza ulifanikiwa kuchanja watoto zaidi ya laki Mbili sawa na asilimia 107 kati ya walengwa waliotarajiwa kuchanjwa ni laki 191,440 wenye umri chini ya mwaka mmoja, tumefikia malengo na kuyavuka,” anasema. 

Mkazi wa Jiji la Mwanza Amina Said, anasema kutolewa kwa chanjo hiyo ni moja ya mapambano ya kumkinga mtoto wa kike asipate saratani ya mlango wa kizazi. 

Anasema elimu juu ya chanjo hiyo inatakiwa kutolewa mara kwa mara ili jamii iendelee kuelewa umuhimu wa chanjo hiyo. 

"Mimi nina mtoto wa kike ana umri wa miaka name,lakini sina  elimu yoyote, kuwa anapofikisha miaka tisa anatakiwa kupatiwa chanjo hiyo," anasema. 

Anaongeza kuwa, serikali inapambana kuwahakikishia wananchi wake wawe na afya njema, hivyo ana rai elimu iendelee kutolewa kwa jamii, ijue umuhimu wa chanjo. 

Aziza Jumanne, mkazi wa Mwanza anaitaja chanjo hiyo kuwa mkombozi kwa wasichana wenye sifa ya kupata chanjo hiyo, akiishauri jamii izingatie jinsi ya kuwasaidia watoto wa kike wasipate ugonjwa huo. 

"Kila mzazi ambaye ana mtoto wa kike aliye na sifa za kupata chanjo, awapeleke kupata chanjo hiyo," anasema, kuwa watoto wanapopatiwa chanjo, wananudhurika kwa maradhi hayo.

 Anthony Andrew, mkazi wa Maduka Tisa, jijini Mwanza anasema ni wakati wa wazazi na walezi kuachana na mila potofu dhidi ya kuwapo chanjo hizo na kinachotakiwa ni kuisaidia serikali, ili watoto wapate waelewe.

 Andrew anakumbusha chanjo inatolewa bure na inabaki  jukumu la walezi na wazazi kujitokeza na watoto wao waweze kupatiwa chanjo hiyo. 

"Tumekuwa tunasikia kutoka kwa wataalamu wetu wa afya, magonjwa sugu yanayo changia vifo kwa jamii. Katika magonjwa hayo, saratani nayo ipo," anasema, akiwa na ufafanuzi.

 Anaongeza kuwa, saratani zote zina changamoto zake, kama mtu atachelewa kupata matibabu kwa wakati anayonafasi kubwa ya kupoteza maisha.













Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza, wakiwa katika maadhimisho ya chanjo ya HPV, katika viwanja vya Furahisha.
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza, wakiwa katika maadhimisho ya chanjo ya HPV, katika viwanja vya Furahisha.
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza, wakiwa katika maadhimisho ya chanjo ya HPV, katika viwanja vya Furahisha.
Sehemu ya baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za Jiji la Mwanza, wakiwa katika maadhimisho ya chanjo ya HPV, katika viwanja vya Furahisha.
Sehemu ya waandishi wa habari wakichukuwa matukio na taarifa katika maadhimisho ya chanjo ya HPV,  viwanja vya Furahisha Mwanza.
Binti aliyetia fora katika uwasilishaji wa shairi lenye kutia hamasa kwa wazazi kushiriki vyema kuhakikisha watoto wanapatiwa chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi, wakiwa katika Uzinduzi wa maadhimisho ya chanjo ya HPV, katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.
Sehemu ya baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za Jiji la Mwanza, wakiwa katika maadhimisho ya chanjo ya HPV, katika viwanja vya Furahisha.
Sehemu ya baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za Jiji la Mwanza, wakiwa katika maadhimisho ya chanjo ya HPV, katika viwanja vya Furahisha.
Kutoka Bujora ni kundi la ngoma likinogesha shughuli katika maadhimisho ya chanjo ya HPV, viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.